Mashabiki wa Manchester United, wameitaka klabu kuhakikisha “inabonga” na mshambuliaji wake kinda Marcus Rashford ili apewe mkataba mrefu.
Mashabiki hao kupitia mtandao wa Twitter, wamesisitiza Man United ihakikisha mwanafunzi huyo wa shule ya Ashton-on-Mersey.
Mkataba wa sass wa Rashford unaisha 2017 wakati wa majira ya joto na amekuwa akilipwa pauni 1,500 kwa wiki.
Lakini tayari kuna taarifa uongozi Manchester United umeishaanza mipango ya kumuongezea mkataba mpya ambao atakuwa akilipwa pauni 15,000 kwa wiki ambayo ni mara 10 ya mshahara wake.
Hofu kubwa kwa mashabiki hao kama Manchester United ikizubaa, inaweza kupokonywa tonge mdomoni kijana akachukuliwa.
Rashford mwenye miaka 18 amekuwa gumzo zaidi baada ya kufunga mabao mawili katika mechi yake dhidi ya Arsenal ambapo Man United ilishinda kwa mabao 3-2 wikiendi iliyopita.









0 COMMENTS:
Post a Comment