Uongozi wa Yanga umeamua kwenda na mtindo wake uleule wa kimyakimya wakati wa maandalizi yake dhidi ya Azam FC.
Tayari kikosi cha Yanga chini ya Mholanzi, Hans van der Pluijm, tayari kipo mjini Pemba ambako kimeweka kambi kujiandaa na mechi hiyo ya Jumapili ijayo.
Yanga itaivaa Azam FC katika mechi kali ya Ligi Kuu Bara na Jangwani wataendelea kufanya mambo yao kimyakimya.
“Tunaweza kuzungumza, lakini bado ukimya kwenye mambo yetu mengi utaendelea. Hii ndiyo staili yetu,” alisema Mkuu wa habari na msemaji wa Yanga, Jerry Muro.
Mara ya mwisho, Yanga ilikuwa mjini Pemba ambako iliweka kambi kwa lengo la kushinda dhidi ya watani wake, Simba na ikafanikiwa kufanya hivyo kwa kuwaangusha kwa mabao 2-0.







0 COMMENTS:
Post a Comment