March 29, 2016


Kocha wa Simba, Jackson Mayanja amewataka watu kuachana na hisia za yeye amekorofishana na nani au atakorofishana na yupi.

Badala yake wafikirie zaidi maendeleo ya Simba ambayo sasa inapambana kupata ubingwa.

“Sina ugomvi na mtu hata mmoja, akili yangu ni kuhakikisha Simba inafanya vizuri kwa kushirikiana na wenzangu wote hadi uongozi.

“Lakini kama atatokea mtu akafanya mambo ya utovu wa nidhamu, basi ajue hakutakuwa na mchezo, sitakubali,” alisema.

Mayanja aliingia kwenye mtafaruku na Hassan Isihaka ambaye alimjibu kocha huyo maneno yasiyo ya kiungwana.


Baadaye akafuatia Abdi Banda na Mayanja amesisitiza wote kuadhibiwa, jambo ambalo limesifiwa sana na wadau hasa kutokana na tabia yake ya kushikilia nidhamu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV