March 22, 2016


Kikosi cha Simba kinatarajia kuendelea na mazoezi kesho ikiwa ni baada ya siku tatu za mapumziko.

Simba imepumzika kwa siku hiyo mara baada ya mechi dhidi ya Coastal Union ambayo waliitwanga kwa mabao 2-0 kwao Tanga, Jumamosi.

Baada ya hapo, Kocha Mkuu, Jackson Mayanja alitangaza mapumziko ya siku tatu hadi kesho.

Siku ya pili ambayo ni Jumapili, Simba waliitumia kwa safari kurejea Dar es Salaam na kesho maandalizi ya kuivaa Majimaji yataanza.


Simba ndiyo vinara wa Ligi Kuu Bara wakiwa na pointi 57, wakifuatiwa na Yanga, Azam FC zote kila moja ikiwa na pointi 50.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV