March 22, 2016

Kocha wa Yanga, Hans van der Pluijm amewataka wadau wa soka nchini wasitake kuwatisha.

Pluijm raia wa Uholanzi, amesema kuwavaa Al Ahly ni kazi ngumu lakini Yanga ni timu kubwa, hivyo haipaswi kuogopa, badala yake inapaswa kujiandaa.

“Tunapaswa kujiandaa, si kuwa wenye hofu au tuliochanganyikiwa. Hii si mara ya kwanza kukutana na Al Ahly,” alisema.

“Hakuna mtu asiyejua Al Ahly ni bora, lakini kila unavyozidi kwenda mbele kwenye michuano yoyote ndiyo unakutana na timu bora.”


Yanga inakutana na Al Ahly katika hatua ya pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuzing’oa Cercle de Joachim ya Mauritius na APR ya Rwanda.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV