March 21, 2016

ULIMWENGU NA SAMATTA
Mshambuliaji nyota wa TP Mazembe, Thomas Ulimwengu anatarajia kuungana na kikosi cha Taifa Stars leo mjini ND’jamena nchini Chad.

Stars imetua nchini humo jana tayari kwa mechi yake ya kuwania kufuzu kucheza Kombe la Mataifa Afrika inayotarajia kupigwa keshokutwa.

Ulimwengu anatarajia kutua nchini humo leo akitokea DR Congo ambako aliitumikia timu yake jana katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.


“Nitaungana na wenzangu hukohuko Chad,” alisema Ulimwengu alipozungumza na SALEHJEMBE kutoka DR Congo.

Mshambuliaji mwingine na nahodha wa Stars, Mbwana Samatta naye ataungana na wenzake moja kwa moja akitokea nchini Ubelgiji ambako anakipiga katika timu ya KRC Genk.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV