March 22, 2016



Kocha Mkuu wa Real Madrid, Zinedine Zidane raia wa Ufaransa amesema kikosi chake kipo tayari kwa ajili ya mechi dhidi ya wapinzani wao wakubwa Barcelona.

Mechi inayozikutanisha Barcelona na Madrid inajulikana kama El Clasico na ndiye mechi maarufu zaidi za watani kisoka kuliko zote duniani.

Mechi hiyo imepangwa kupingwa Aprili 2 na Zidane amesema kikosi chake kipo tayari na hasa kama kitaendelea na uchezaji kama wa mechi iliyopita.

Katika mechi iliyopita, Real Madrid iliitwanga Sevilla kwa mabao 4-0 na Zidane akasema anataka timu yake icheze namna ile.


Presha kubwa kwa gwiji hilo la Real Madrid ni mechi dhidi ya Barcelona ambayo itakuwa ni El Clasico yake ya kwanza akiwa kocha.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic