Cheki taswira, kinda wa Azam FC, Farid Mussa akiwa katika majaribio kuwania nafasi acheze soka la kulipwa barani Ulaya. Hapa Farid anafanya majaribio katika klabu ya Club Deportivo Tenerife Hispania. Leo ametimiza siku ya nne katika majaribio na taarifa zinasema anaendelea vizuri.
Awali, Farid alisema ana imani kubwa kwamba atapasi majaribio hayo kwa kuwa ndiyo kitu alichokuwa anakihitaji na atakipigania kwa nguvu zote.
Hata hivyo, Farid alikubali kwamba anaona Hispania wamepiga hatua kubwa kimaendeleo katika soka, jambo ambalo ni zuri kwake kwa kuwa atajifunza zaidi.
PICHA KWA HISANI YA AZAM FC.
0 COMMENTS:
Post a Comment