April 4, 2016


Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe amesema anashangazwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kufanya waziwazi upendeleo kwa Yanga, likionyesha wazi limepania kuisaidia kuwa bingwa.


Akizungumza katika mahojiano maalum na Salehjembe, Hans Poppe amesema mechi ya Yanga dhidi ya Mtibwa Sugar iliyokuwa ichezwe Aprili 6, imesogezwa hadi Aprili 16, jambo ambalo ni ujanja kwa kuwa itaahirishwa tena ili Yanga iendelee kuwa na viporo.

Hans Poppe amefafanua hivi: 
Salehjembe: Imesogezwa hadi Aprili 16, sasa hofu yako ni ipi na unajua Yanga ina majukumu ya kimataifa?
Hans Poppe: Kama Yanga wameshindwa kucheza Aprili 6, swali la kwanza jiulize, mbona Azam FC watacheza dhidi ya Ndanda. Lakini Kupelekwa Aprili 16 ni danganya toto.

Salehjembe: Danganya toto kivipi Hans Poppe?
Hans Poppe: Yanga watakuwa na mechi ya marudiano na Al Ahly kati ya Aprili 19 na 20. Katika hali ya kawaida, watakuwa wanaondoka kati ya Aprili 15 au 16 kwenda Misri. Hauwezi kuniambia watacheza.

Salehjembe: Lakini hilo hauna uhakika?
Hans Poppe: Uhakika unakuja hivi, Aprili 16 hadi 19 ni siku tatu. Lakini Aprili 6 hadi Aprili 9 ni hivyohivyo. Sasa kama siku ziko sawa, kwa nini hawakucheza mechi ya Mtibwa Aprili 9?

Salehjembe: Fafanua kidogo msomaji akuelewe, tafadhari..
Hans Poppe: Utaona Yanga wameacha kucheza katika kipindi cha tofauti ya siku tatu hadi wanapokutana na Al Ahly, mechi imesogezwa mbele. Sasa Aprili 19 au 20 watakuwa na mechi ya ugenini inayojumlisha wao kusafiri, unafikiri watacheza vipi? Kwa nini wasingecheza mechi hii ya nyumbani ambayo haijumuishi safari?

Salehjembe: Kwa hiyo unafikiri kipi kitatokea?
Hans Poppe: Ndiyo maana nimesema, hata hiyo mechi imepangiwa siku ambayo itasogezwa tena kwa kisingizio kilekile ili Yanga iendelee kuwa na mechi za viporo mbele.

Salehjembe: Lakini kwa nini unaonekana kuwa na hofu na viporo wakati Simba inakusanya pointi zake kwa uhakika?
Hans Poppe: Kiporo mwishoni kwa timu zinazochuana kileleni ni hatari, hii ni rahisi sana watu kuingia kwenye ushawishi wa upangaji matokeo. 


Vizuri timu zingemaliza mechi zao kwa pamoja na kufanya mambo yawe “fea”. Lakini si wengine kutengeneza mazingira ambayo yanaonyesha TFF tayari wana bingwa wao. 
Hii si haki, hii si sawasawa na hili jambo linaonyesha kiasi gani hakuna haki katika mpira wa Tanzania. Nimekuwa nikisema sana lakini naonekana kama mkorofi, lakini sasa mambo yanakwenda hadharani na kila kitu kinaonekana bila hata tabu au kulazimika kupiga hesabu kwamba TFF imejipanga kupata bingwa wake.

2 COMMENTS:

  1. Si jana tu aliwaambia wenzie waache kulalamika badala yake wacheze mpira!? Sa mbona yeye analalamika!? Na yeye aache kulalamika ashinde mechi zake zote!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Huyu jamaa kaingia katika soka kwa bahati mbaya naona anataka kuficha yale maovu yake,sisi tunamfahamu yeye ni mtu wa mtutu ndio maana akatuhumiwa kutaka kumdedisha mwalim nyerere.

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic