April 30, 2016


Kiungo Haruna Niyonzima wa Yanga amesema timu yake haina muda wa kupoteza katika mechi zilizobaki za Ligi Kuu Bara na leo watahakikisha wanaifunga Toto Africans kisha kuwahi mchezo mwingine.

Yanga imebakisha mechi tano tu za ligi kuu kuanzia hii ya leo, kisha itacheza na Stand United mkoani Shinyanga halafu Mbeya City na Majimaji na itamaliza na Ndanda FC mjini Mtwara.

Niyonzima raia wa Rwanda aliliambia Championi Jumamosi kuwa, hawana muda wa kupoteza jijini hapa zaidi ya kuifunga Toto Africans halafu kuwaza mchezo mwingine unaofuata. 

“Kutokana na kasi tuliyonayo, hatuna muda wa kupoteza tunachohitaji katika mchezo huu ni kushinda halafu tuwaze mechi inayofuata, lengo letu ni kutetea ubingwa.

“Tunajua Toto iliifunga Simba, lakini hiyo si sababu ya kuwaachia wacheze wanavyotaka tutapambana kupata pointi tatu ili mambo yetu yaende vizuri,” alisema Niyonzima. 


Yanga ambayo jana ilifanya mazoezi kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, ipo kileleni mwa ligi kuu ikiwa na pointi 62 wakati Toto Africans ipo nafasi ya 11 ikiwa na pointi 30.

SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV