April 29, 2016



Straika hatari wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, Kipre Tchetche, yupo fiti asilimia 100 kuivaa Simba  kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) utakaopigwa keshokutwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Tchetche aliyeanza mazoezi hivi karibuni alikuwa akisumbuliwa na maumivu ya enka aliyopata kwenye mechi ya ligi kuu dhidi ya Mtibwa Sugar uliopigwa kwenye Uwanja wa Manungu, Morogoro ambao Azam FC ilishinda bao 1-0 lililofungwa kwa mkwaju wa penalti na nahodha John Bocco ‘Adebayor’.

Kocha Mkuu wa timu hiyo, Stewart Hall, amethibitisha kuwa Tchetche yupo fiti kwa ajili ya mchezo huo baada ya kupona majeraha yaliyokuwa yakimkabili.

Katika hatua nyingine kiungo Frank Domayo, aliyepata maumivu ya enka wakati wa mchezo wa Mwadui, yeye atakuwa fiti baada ya wiki mbili zijazo na sasa anaendelea na matibabu chini ya jopo la madaktari wa Azam FC.

Kuhusu uwepo wa wachezaji wengine kama vile Pascal Wawa, Allan Wanga, Wazir Salum, Racine Diouf  itajulikana mara baada ya mazoezi ya mwisho ya Azam FC kesho kabla ya kuwavaa Wekundu hao wa Msimbazi.

Kiungo Himid Mao 'Ninja' yeye ataendelea kukosekana kutokana na kutumikia adhabu ya kadi nyekundu aliyoipata kwenye mchezo namba 170 dhidi ya Mtibwa Sugar.


Azam FC iliyobakisha michezo mitano ya ligi, mpaka sasa inashika nafasi ya pili kwenye msimamo ikiwa imejikusanyia pointi 58, Simba yenyewe imejizolea pointi 57 katika nafasi ya tatu huku Yanga ikiwa kileleni baada ya kufikisha pointi 62.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic