April 30, 2016


MWADUI FC
Kikosi cha Mwadui FC kimedhihirisha kwamba ni wababe wa mji wa Shinyanga baada ya kuwatwanga wapinzani wao wakubwa kwenye mji huo Stand United kwa mabao 2-1.

Mwadui FC inayofundishwa na Jamhuri Kiwhelo ‘julio’ ndiyo iliyoonyesha soka safi zaidi na kufanikiwa kupata ushindi huo.

Ligi hiyo pia iliendelea mjini Mbeya kwa Prisons kuwakaribisha JKT Ruvu ambao walikomaa na kupata sare ya 1-1.


Mbeya City wakiwa wageni wa Mtibwa Sugar pale Manungu licha ya kuonyesha soka safi na kukomaa kinoma lakini wakachapwa kwa bao 1-0.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV