April 27, 2016Mshambuliaji wa Atletico Madrid, Fernando Torres amesema kikosi chao kilo tayari kwa mechi ngumu ya kesho dhidi ya Bayern Munich.

Nusu fainali ya pili ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, inasubiriwa kesho kwa hamu kubwa jijini Madrid lakini Torres amesema wake tayari kuandika historia nyingine.

“Tuko tayari kuandika historia mpya, tuko tayari kupambana na tunaisubiri siku hiyo kwa hamu,” alisema Torres.


Atletico ambayo imesherekea miaka 113 tokea kuanzishwa kwake imekuwa moja ya timu tishio katika kipindi hiki.

Nusu fainali ya kwanza, imechezwa leo na Real Madrid ikiwa ugenini imepata sare ya 0-0 dhidi ya Manchester City.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV