May 15, 2016


Mechi kati ya Manchester United dhidi ya Bournemouth iliahirishwa baada ya kudaiwa kuna mzigo uliozua hofu huenda ukawa bomu.

Kwanza mashabiki wapatao 20,000 waliokuwa upande wa jukwaa moja wakatolewa kwenye Uwanja Old Trafford. Baadaye Jeshi la Polisi likashauri mashabiki wote watolewe.

Lakini mbwa ndiyo walifanya kazi kubwa ya ziada kuhakikisha usalama na kuthibitisha kuhusiana na hofu hiyo.

Baadaye lilipatikana begi hilo, hata hivyo baada ya ukaguzi ilielezwa halikuwa bomu.
0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV