May 21, 2016Nahodha wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ amesema kama wasingetulia na kutumia uzoefu, vituko vya wapinzani wao Sagrada Esperanca vingewatoa mchezoni na wangetolewa katika Kombe la Shirikisho.

Akizungumza muda mfupi baada ya kurejea nchini jana akitokea Angola na Yanga, Cannavaro alisema Esperanca walipanga kuwatoa mchezoni makusudi ili wawafunge mabao mengi.

“Walianza uwanja wa ndege vituko vikawa vingi ambapo mwenzetu Ngoma (Donald) alipoteza begi, mambo mengi waliyaweka hovyo makusudi.

“Kutokana na uzoefu wangu na wenzangu tulijitahidi kuwaweka sawa wenzetu kisaikolojia na tukafanikiwa japokuwa tulifungwa bao moja tu,” alisema Cannavaro.

“Pia tunaushukuru uongozi kwa kazi nzuri waliyoifanya ya kutuwezesha muda wote na kufika hatua hii ya kucheza hatua ya makundi Kombe la Shirikisho Afrika.”


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV