May 21, 2016


Kwa mujibu wa Rais wa Simba, Evans Aveva, kitendo cha wachezaji wake watano wa kigeni kuweka mgomo ni sawa na kuvunja mikataba yao wenyewe. 

Wachezaji hao wa kigeni ni Hamisi Kiiza, Juuko Murshid, Brian Majwega (wote raia wa Waganda), Emery Nimubona (Burundi) na Paul Kiongera wa Kenya.

Hao waligomea safari ya kwenda Ruvuma kucheza na Majimaji wakishinikiza walipwe mishahara yao, iliyokuwa imepitisha siku tisa. 

Aveva alisema, kitendo walichofanya wachezaji hao ni kukiuka mikataba yao na kwamba uongozi umewaandikia barua za kujieleza kisha kamati ya nidhamu itakaa kusikiliza utetezi wao.

 “Kitendo walichofanya ni kuvunja mkataba, tumewataka kila mmoja ajieleze kwa maandishi sababu za kuvunja mikataba kwani waligoma na kamati ya nidhamu itakuwa na majibu ya hatima yao,” alisema rais huyo aliyeingia madarakani miaka miwili iliyopita.

Aveva alisema hadi juzi ni Kiiza tu aliyeitikia suala hilo kwa kufika ofisini kwake kujua hatima yake na kuchukua barua hizo, huku beki Emery akisema hana taarifa zozote.
Kiiza hakuwa tayari kuzungumzia sakata hilo kwa maelezo kuwa linashughulikiwa na uongozi.


1 COMMENTS:

  1. Kuvunja mkataba ni kukiuka mashart ya mkataba, nani aliyeanza!? ambaye hakulipa mshahara au aliyegoma kufanya kazi kabla ya kutimiziwa matakwa ya ambacho ameshakifanyia kazi!? Tuache siasa, bila hivyo hatuwezi piga hatua

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV