May 25, 2016


Bondia wa ngumi za kulipwa nchini, Francis Cheka, amefunguka kuwa kamwe hataweza kusaini mkataba wa aina yoyote ambao utakuwa chini ya milioni kumi baada ya hivi karibuni kutaka kusainishwa mkataba akiwa amelewa ili acheze na Abdallah Pazi ‘Dulla Mbabe’.

Cheka amesema kuwa kuna watu wamekuwa wanatangaza atacheza na Dulla Mbabe kitu ambacho hakiwezekani kutokana na kuwa katika nafasi tofauti huku wakitaka kumletea ujanja katika mkataba wenyewe.

“Wanataka nicheze na Dulla lakini haiwezekani, kwanza hajafikia viwango vyangu, halafu wanajifanya wajanja, waliniletea mkataba wao wa milioni 8 nikiwa nimelewa, wakajua nitausaini ila nikagomea na haitawezekana, maana wao wanataka kutumia mabondia ili wafaidike,” alisema Cheka.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV