Ile ishu ya makocha wapya wa Azam, Zeben Hernandez na Jonas Garcia kushindwa kuinoa timu hiyo mara baada ya kuingia mkataba ni kutokana na kukosa vibali vya kufanyia kazi Tanzania.
Hernandez ambaye ni kocha mkuu aliyerithi mikoba ya Muingereza, Stewart Hall huku Garcia akiwa ni mtaalamu wa viungo, wameingia mkataba wa mwaka mmoja wa kuitumikia timu hiyo ambapo wataanza kazi rasmi Julai, mwaka huu kwenye michuano ya Kombe la Kagame.
Mtendaji Mkuu wa Azam, Saad Kawemba, amesema baada ya kuingia nao makubaliano ya kuinoa timu hiyo, wakawapa ruhusa ya kwenda kwao huku wakiwa wanafuatilia vibali vya kufanyia kazi Tanzania ambapo wanaamini kabla ya kuanza kwa michuano ya Kombe la Kagame, kila kitu kitakuwa sawa.
“Baada ya kumalizana na wale makocha kutoka Hispania, tukawaambia wakapumzike kwanza na hiyo imekuja kutokana na kukosa vibali vya kufanya kazi Tanzania.
“Wasingeweza kufanya kazi bila ya vibali hivyo ambapo kwa sasa tupo kwenye mchakato wa kuwatafutia na tunaamini kabla ya Kombe la Kagame kila kitu kitakuwa sawa,” alisema Kawemba.
0 COMMENTS:
Post a Comment