May 25, 2016


Siku chache kabla ya tamasha maarufu la kila mwaka la Majimaji Selebuka linalotarajiwa kukata utepe Jumamosi wiki hii, zoezi linaloendelea kwa sasa ni usajili wa washiriki wote.

Tamasha hilo linaloratibiwa na Asasi ya Somi, litadumu kwa wiki nzima kuanzia Mei 28, mpaka Juni 4, mwaka huu kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Mashujaa wa Vita vya Majimaji mjini Songea.

Lengo kuu la tamasha hilo ni kuibua vipaji vya michezo, kuuenzi utamaduni wa Mkoa wa Ruvuma, pamoja na kumuinua mwananchi wa kawaida kupitia ujasiriamali.

Mashindano yatakayohusika ni pamoja na mbio za baiskeli, riadha mbio fupi na ndefu, ngoma za asili, maonyesho ya ujasiriamali, utalii wa ndani ukiwemo kutembelea Jumba la Mashujaa wa Vita ya Majimaji pamoja na mdahalo kwa shule za sekondari huku kukiwa na zawadi, medali na cheti kwa washindi wote.


Mratibu wa tamasha hilo, Reinafrida Rwezaura ameiambia SALEHJEMBE kuwa: “Mpaka sasa kinachoendelea ni zoezi la usajili kwa washiriki wote, fomu zinapatikana kwenye tovuti ya www.somi.international pamoja na Ofisi za Maleta&Ndumbaro mjini Songea.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic