May 21, 2016Heshima ya mashujaa walioipa Leicester City ubingwa wa Ligi Kuu England sasa itabaki milele.

Mashujaa hao, kuanzia Kocha Claudio Ranieri na wachezaji wengine, picha zao zimeanza kuchorwa katika kuta za mitaa mbalimbali za mii wa Leicetster.

Wachezaji ambao tayari mchoraji maarufu Richard Wilson ameanza kuwachora ni nahodha Wes Morgan,kipa Kasper Schmeichel na mwanasoka bora wa mwaka wa Ligi Kuu England, Riyad Mahrez.

Imeelezwa, mchoraji huyo maarufu atawachora wachezaji wote lakini akianza na kikosi cha kwanza cha timu hiyo.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV