May 21, 2016



Timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 17, Serengeti Boys wamepata sare nyingine baada ya Malaysia kusawazisha mabao yote mawili waliyotangulia kufunga vijana hao.

Mechi hiyo ni ya michuano ya Kombe la Vijana la AIFF inayofanyika katika mji wa Goa nchini India.

Boys walianza kupata bao lao la kwanza katika dakika ya 31 kupitia mshambuliaji wao hatari, Asad Ali Juma na Yohana Oscar akaongeza la pili katika dakika ya 59, ikiwa ni dakika chache baada ya kuanza kwa kipindi cha pili.

Makosa ya walinzi, yaliwaruhusu Malaysia kusawazisha mabao yote mawili ndani ya dakika tano tu.

Walianza kupata bao la kwanza katika dakika ya 63 kupitia Arif Suhaimi na Najmi Idhar akafunga la pili katika dakika ya 68.

Hii ni sare ya tatu kwa Boys zikiwemo zile za 1-1 dhidi ya Marekani, 2-2 dhidi ya Korea na imepata ushindi mmoja wa mabao 3-1 dhidi ya wenyeji India. Inaendelea kuwa haijapoteza hata mechi moja katika michuano hiyo.

1 COMMENTS:

  1. ubaya ni kwamba watarudi hapa nyumbani na tusijue walipoelekea tena

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic