May 23, 2016

AZAM FC
Chama cha Dar es Salaam (DRFA) kimezipongeza klabu zake tatu za ligi kuu kwa kumaliza katika nafasi za juu kwenye michuano ya ligi kuu soka tanzania bara.

Klabu hizo Yanga SC ambao ndiyo mabingwa wa Ligi Kuu Bara, Azam FC katika nafasi ya pili na Simba walioshika nafasi ya tatu.

Mwenyekiti wa DRFA, Almas Kasongo amesema mafanikio hayo wanayapeleka moja kwa moja kama zawadi kwa mkuu wa mkoa wa Dar  es Salaam, Paul  Makonda ambaye ameonyesha mchango mkubwa kwa kuhimiza watu kupenda michezo.


Amesema kama chama hawana budi kujivunia mafanikio hayo na kuwapongeza wachezaji,walimu na viongozi wa vilabu vyote vitatu kwa hatua hiyo inayozidi kuupamba mkoa wa Dar es Salaam kisoka.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV