June 19, 2016


Pamoja na kwamba awali alionekana kama ameitwa kwa kupendelewa, nahodha wa Man United, Wayne Rooney, sasa anaonekana kuwa ndiye tegemeo katika kikosi cha England hasa katika suala la uchezeshaji.

Rooney ndiye mchezaji aliyepiga pass nyingi zaidi katika kikosi cha England tena akigawa kwa wachezaji wengi zaidi.


Katika mechi mbili za Russia na Wales, Rooney ndiye mchezaji aliyepiga pais nyingi kwa wachezaji 10 tofauti wa England. alipiga jumla ya pasi 114 na kuwa na mafanikio ya 54% zikifanya vema.

Pamoja na England, Rooney anaendelea kuwa kati ya wale waliopiga pasi nyingi zaidi Man United licha ya kucheza mechi chache. Kwa sasa hakuna ubishi kuwa ndiye “moyo” wa kikosi cha England.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV