June 24, 2016



Shirikisho la Soka Afrika (Caf), limetangaza kuindoa ES Setif ya Algeria katika michuano ya Ligi ya Mabingwa.

Caf imetangaza kupitia akaunti yake ya mtandao wa kijamii wa Twitter, kuwa Setif wameondolewa baada ya mashabiki wao kufanya vurugu katika mechi dhidi ya Mamelodi Sundowns maarufu kama Masandawana.

Mashabiki hao walianzisha vurugu kubwa na kusababisha mchezo huo kusimama kwa kipindi kirefu, baadaye mwamuzi akalazimika kumaliza mpira wakati mashabiki walipoamua kurusha mawe, chupa na vitu vingine uwanjani wakionyesha kutofurahishwa kwa kuwa timu yao ilikuwa nyuma kwa mabao 2-0.

Huenda hilo linaweza kuwa funzo kwa mashabiki wa soka nchini hasa wale wa Yanga ambao timu yao inashiriki michuano ya Kombe la Shirikisho, kwamba hawatakiwi kufanya vitendo vya kihuni kwa kuwa Caf, hawana mchezo katika hilo.

Katika hatua ya makundi ES Setif ilikuwa ikitane na Zamalek katika mechi yake ya pili iliyopangwa kupigwa Juni 29 jijini Cairo, Misri lakini sasa safari imewakuta.


1 COMMENTS:

  1. Mbona timu za misri zinafanya fujo na wala haziondolewe mashindanoni?Au ndio kwavile CAF ipo hapo Misri?Hakuna haki mpirani hadi Ulaya mambo ni hayohayo!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic