June 6, 2016



Kiungo wa Chelsea anayecheza kwa mkopo katika Klabu ya  AS Roma, Mohammed Salah, Jumamosi iliyopita alilazimika kuomba jezi ya kiungo wa Taifa Stars, Farid Mussa, kutokana na uwezo aliuonyesha kiungo huyo katika mchezo wa kuwania kufuzu Fainali za Mataifa Afrika dhidi ya  Misri.

 Katika mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar, Stars ilikubali kichapo cha mabao 2-0, yaliyofungwa na straika huyo huku akiwa ndiye mchezaji pekee aliyeweza kubadilishana jezi na mchezaji wa Stars.

 Baada ya zoezi hilo Farid alisema ndiye alikwenda kumuomba wabadilishane jezi  kitendo kilichokubaliwa na kiungo huyo anayetarajia kujiunga na Klabu ya Teneriffe, inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza nchini Hispania.


Farid amesema hakuwa na mpango wa kubadilishana jezi na mchezaji yeyote lakini alipofuatwa na Salah na kuombwa alikubali ombi lake.

“Kukweli kwanza sikupanga kubadilishana jezi na mchezaji yoyote, lakini aliponifuata Salah nikiwa sina jinsi nikakubali kumpa jezi yangu naye akanipa yake,” alisema Farid ambaye alionyesha kiwango cha juu kwenye mechi hiyo..   


1 COMMENTS:

  1. Acha uongo sisi wote tulimwona jinsi Farid alivyokuwa akimnyemelea Farah wakati wa kipenga cha mwisho na kuwahi kuvua jezi yake na kumpa Farah kitendo kilichomlazimu Farah naye kuvua yakwake na kumpa Farid.Yaani wewe ni kanjanja namba moja ku
    wa uongo kumzidi Zubeiry

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic