June 15, 2016
Mashabiki, wadau wa soka, ngudu na jamaa wamejitokeza kwa wingi leo kumuaga Joh Mabula ambaye amefariki dunia siku tatu zilizopita baada ya kushambuliwa kwa kuchomwa kisu.

Mabula aliuwawa katika eneo la Kitunda jijini Dar es Salaam wakati akiamua ugomvi wa shemeji yake dhidi ya muuaji huyo ambaye inaelezwa alikimbilia katika enero la Bagamoyo na msako ni mkali sana dhidi ya yake.


Shughuli za kuuaga mwili wake zilifanyika nyumbani kwake Kitunda, Kibeberu na baada ya hapo mwili wake ulisafirishwa mjini Shinyanga kwa ajili ya mazishi.


Mshambuliaji huyo alimuua Mabula pamoja na shemeji yake chanzo kikielezwa shemeji yake kupita mbele ya runinga wakati muuaji alikuwa akiangalia na wenzake.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV