June 14, 2016


Beki wa kulia wa Yanga, Juma Abdul Jaffar ambaye ukoo wake ni Mnyamani anatarajia kurejea uwanjani mapema kuliko ilivyotarajiwa.

Awali, Juma alitarajiwa kurejea uwanjani na kuanza mazoezi ya taratibu lakini sasa inawezekana ikawa mapema zaidi.

“Anaonekana kuendelea vizuri, anapona haraka na huenda atarejea haraka uwanjani,” alisema mmoja wa madaktari wanaomsimamia.


Lakini awali, Juma alisema: “Inategemea na hali yenyewe, kuwa ninaendeleaje. Ninaamini nitarejea uwanjani mapema zaidi.”

Kikosi cha Yanga kipo nchini Uturuki ambako kimeweka kambi kujiandaa na mechi yake ya kwanza ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Mo Bejaia ya nchini Algeria.

Beki huyo alibaki nchini ili aendelee na matibabu, hii ilitokana na yeye kuumia wakati akiichezea Taifa Stars katika mechi dhidi ya Misri.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV