June 15, 2016


Beki wa kulia wa Yanga, Hassan Kessy, ametamka kuwa kambi yao ya nchini Uturuki, anaamini itamfanya aongeze kiwango chake na kuwa na makali zaidi kwa msimu ujao wa Ligi Kuu Bara na michuano ya kimataifa.

Yanga kwa sasa ipo nchini Uturuki kwa kambi ya muda kabla ya kwenda Algeria kucheza mechi yao ya kwanza ya hatua ya makundi katika Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya MO Bejaia.

Kessy ambaye naye yupo kambini huko sambamba na nyota wengine wanne waliosajiliwa na Yanga hivi karibuni, Juma Mahadhi, Andrew Vincent ‘Dante’ na Beno Kakolanya, alisema kuwa nafasi ya kusafiri na kikosi aliyoipata itamfanya kumuongezea namna ya kuwasoma zaidi wenzake ili siku ya mechi ikifika asiwe kama mgeni.

“Kwa upande wangu nina furaha kuona kwamba nimesafiri na kikosi licha ya kuwa ndiyo kwanza nimeingia hivi karibuni, lakini jambo hilo linaonyesha kwa kiasi gani benchi la ufundi lilivyo na imani na mimi, niseme tu kuwa sitawaangusha.


“Naamini kwa kupitia kambi hii ya Uturuki nitaweza kujifunza mambo mengi ya Yanga ikiwemo mbinu, aina ya uchezaji na mambo mengine ambayo yatanifanya nizidi kukiboresha kiwango changu na nina uhakika mara baada ya kambi hii.

"Nitakuwa moto zaidi na nitaisaidia timu yangu kufanya vizuri katika michuano ya Kombe la Shirikisho na Ligi Kuu Bara msimu ujao,” alisema Kessy.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic