June 18, 2016

CHIRWA NA NGOMA WAKISHEREKEA BAO WAKATI WAKIWA FC PLATINUMS YA ZIMBABWE
Kiroho safi straika Donald Ngoma ameelezwa kupendekeza usajili wa straika Obrey Chirwa katika klabu yake ya Yanga akimtosa Walter Musona aliyekuwa chaguo lingine la timu hiyo.

Yanga ilikuwa na mpango wa kusajili straika mwingine wa kigeni baada ya kutoridhishwa na uwezo wa Issouf Boubacar raia wa Niger, hivyo ikawa na chaguo la kwanza Danny Phiri ‘Deco’ wa Chicken Inn ya Zimbabwe.

CHIRWA WAKATI AKITUA DAR, JANA.
Chaguo la pili la Yanga lilikuwa Chirwa wa FC Platinum pia ya Zimbabwe na la tatu lilikuwa ni Walter Musona pia wa Platinum.

Bosi mmoja wa Yanga anayeshughulikia mambo ya usajili aliliambia Championi Jumamosi kuwa, baada ya kushindwa kumsajili Deco, Ngoma aliwashauri kuhakikisha anasajiliwa Chirwa badala ya Musona.

“Ni jambo la ajabu kabisa kwani Ngoma alitueleza kuwa ni bora tumsajili Chirwa ambaye ni raia wa Zambia kuliko Musona ambaye ni Mzimbabwe mwenzake.

“Tulishangaa kwani tulidhani labda angempendekeza raia mwenzake wa Zimbabwe, (Ngoma) alitueleza Chirwa ni mzuri zaidi ya Musona, na sisi tukafuata ushauri wake,” alisema bosi huyo.


Chirwa aliwasili nchini jana jioni na alikuwa na mazungumzo ya mwisho na uongozi wa Yanga jioni hiyo kabla ya kusajiliwa halafu leo ataenda Algeria kujiunga na kikosi cha timu hiyo ambacho kesho kinacheza na MO Bejaia katika Kombe la Shirikisho Afrika.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic