June 6, 2016



Taarifa kwa umma
Rais wa klabu ya Simba Evans Aveva anayo furaha kubwa ya kuwatakia waislaam wote nchini maandalizi mema ya nguzo ya nne ya dini ya kiislaam kufunga swaumu ya Ramadhan.

Katika salaam zake za ibada hiyo muhimu Rais Aveva amewaomba wanachama na washabiki wa Simba kutumia 'fardhi' hiyo muhimu kuendelea kuiombea klabu ambayo ipo kwenye mchakato muhimu wa usajili wa wachezaji na pia maandalizi ya mkutano mkuu wa mwaka utakaofanyika mwezi ujao tarehe kumi.

Kwenye salaam hizo pia amewaomba waislaam kuongeza ibada kwa mola wao kama walivyoamrishwa katika kitabu kitukufu cha Qur-ani.

"Ni matumaini yangu kuwa Ramadhani hii itaendelea kutuunganisha wanasimba na wapenda michezo kote nchini," alisema Aveva katika salamu hizo kwa mashabiki, wanachama wa Simba, wapenda michezo na umma kwa ujumla.


Imetolewa na
Haji S.Manara
Mkuu wa habari, Simba Sports Club

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic