July 6, 2016


Baada ya kuachwa na ndege, hatimaye kipa namba moja wa Simba, Vincent Angban raia wa Ivory Coast, ametua nchini.

Angban alitakiwa kutua nchini, Jumapili iliyopita akiambatana na mshambuliaji raia mwenzake wa Ivory Coast ambaye anatarajiwa kusajiliwa na Simba, Blagnon Goue Fredric, lakini alishindwa kufanya hivyo baada ya kudaiwa kuchelewa ndege.

Hata hivyo, Fredric ambaye ni mshambuliaji yeye alitua peke yake siku hiyo ya Jumapili na kupokelewa na viongozi wa timu hiyo ambao  tayari wanadaiwa kufanya naye mazungumzo ya awali na kinachosubiriwa sasa ni kuangaliwa uwezo wake na Omog ndipo aweze kusajiliwa.

Akizunguza Meneja wa Simba, Abassi Ally alisema kuwa Angban ametua juzi Jumatatu na kwenda moja kwa moja kuonana na viongozi wa timu hiyo.


“Ni kweli kabisa alitakiwa atue jana lakini alichelewa ndege, hata hivyo tunamshukuru Mungu kwani tayari ameshafika hivyo mashabiki wetu wasiwe na wasiwasi ameshaonanana kocha pamoja na viongozi,” alisema Ally.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV