July 8, 2016


Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa Yanga, Jerry Muro amefungiwa kufanya shughuli za mpira kwa mwaka mmoja. Adhabu hiyo hiyo imetolewa na Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF).

Lakini baada ya kuipokea taarifa hiyo, Muro ameiambia haya SALEHJEMBE:

“Bado niko Machame mapumzikoni, si unajua hiki ni kipindi cha mapumziko. Lakini niwakumbushe mimi mwajiri wangu ni Yanga, si TFF.

“Nitasikiliza mwajili wangu anasemaje, kama ikiwa ni kukaa kimya nitafanya hivyo. Akisema endelea, basi nitakuwa sina namna.


“Sasa nakaa kimya, nitamsubiri mwajiri wangu atakachoniambia. Hivyo kwa sasa acha niishie hapa.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV