July 8, 2016


Saa chache baada ya Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kutangaza kumfungia mwaka mmoja Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano cha Yanga, Jerry Muro, bahati mbaya kapata balaa jingine.

Muro amekumbana na ajali ya gari akiwa njiani kutoka Machame kijijini kwenda Machame mjini ambako yuko mapumzikoni.

Gari alilokuwa akiendesha liliteleza na kwenda kugonga kwenye karavati na tairi kupasuka.

“Hakika nimenusurika, unajua huku Machame ni milima. Halafu sasa kuna utelezi kutokana na mvua ingawa si kubwa, sasa wakati najteremka gari likatereza na kwenda kugonga lile karavati,” alisema Muro.

“Lakini namshukuru Mungu, nimepona. Nilipata shida kupiga jeki kwenye tope mwisho nimefanikiwa na baada ya hapo nitaanza safari ya kwenda Dar es Salaam.”


Muro amefungiwa bila ya kupata nafasi ya kujitetea kwa kuwa wakati barua ya wito kwenda TFF kwa ajili ya kusikilizwa inapelekwa, yeye alikuwa Machame mapumzikoni kwa ajili ya mapumziko ya sikukuu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV