July 16, 2016Beki mpya wa Simba, Emmanuel Semwanza amepata msiba kubwa baada ya kufiwa na mama yake mzazi.

Semwanza ambaye amejiunga na Simba akitokea Mwadui FC inayofundishwa na Jamhuri Kihwelo 'Julio'. Tayari ameondoka kambini kwenda Tunduma, Mbeya kwa ajili ya msiba.

“Kweli ameondoka kambini, tumeelezwa amefiwa na mama yake mzazi,” alieleza mmoja wa wachezaji wa Simba walio katika kambi ya timu hiyo mkoani Morogoro.


Semwanza ni kati ya mabeki wa kati ambao Simba inawatumaini kuimarisha kikosi chao kwa ajili ya msimu ujao.

Juhudi za kumpata Semwanza zilikwama kwa kuwa inaonekana simu yake kuwa imezimwa muda wote.

SALEHJEMBE inatoa pole kwa Semwanza kutokana na msiba huo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV