July 9, 2016


Maendeleo mazuri ya Wakongomani Besala Janvier Bukungu na mwenzake Moussa Ndusha katika mazoezi ya Simba, kumeamsha matumaini zaidi ya kupatikana wachezaji wa kigeni wenye msaada mkubwa.

Bukungu na Ndusha wamekuwa wakiendelea na mazoezi yaliyo chini ya Kocha mpya, Joseph Omog.

Juhudi, uwezo wa kufuata maelekezo ya mwalimu na namna ya uchezaji, kumemfanya kocha huyo kuzidi kuwafurahia.

“Kweli jamaa wanajitoa, wanaonekana wanataka kweli kusajiliwa na kufanya kazi,” kilieleza chanzo.

“Achana na kocha kufurahishwa nao, hata sisi tumekuwa tunavutiwa nao maana ni watu wenye ushirikiano.”

Bukungu aliwahi kuichezea TP Mazembe na ndiye alisababisha ikatiwe rufaa na Simba na kuondolewa katika michuano ya Afrika na nafasi hiyo wakaichukua Simba ambao walishindwa kuvuka kisiki cha Waarabu kwenda kwenye makundi.


Ndusha alikuwa kiungo wa Polisi Rwanda pia alishiriki michuano ya Chan iliyofanyika nchini Rwanda.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV