July 14, 2016


Thamani ya matibabu ya Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Haji Manara imefikia zaidi ya dola 10,000 (zaidi ya Sh milioni 22).

Taarifa za uhakika zinaeleza, Manara ambaye sasa jina lake la kushoto halioni hata kidogo  na la kulia limepungua uwezo wa kuona, gharama imeonekana kupanda kwa kuwa anatakiwa kuchukuliwa vipimo tena mara baada ya kuwasili nchini India.

Manara anatarajia kuondoka nchini Jumamosi kwenda India na shughuli ya uchukuliwaji vipimo itaanza Jumatatu kama kila kitu kitakwenda katika mpangilio.

Tayari Kundi la Mashabiki na Wanachama wa Yanga limejitokeza kumchangia Sh milioni 1 na ushee.

Lakini viongozi wa klabu ya Simba na wale wa Friends of Simba wameelezwa kuwa naye bega kwa bega ili kuhakikisha kila jambo linafanikiwa.


Manara aliamka asubuhi tu jicho lake likiwa limepoteza uwezo wa kuona.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV