July 14, 2016


Kocha Joseph Omog, ameendelea na mazoezi na kikosi chake cha Simba huku akitaka kila kitu kiwe siri.

Simba imeweka kambi mjini Morogoro kujiandaa na Ligi Kuu Bara.

Tokea ametua nchini, Omog amekuwa akisisitiza suala la wachezaji wake kufanya mazoezi bila ya mashabiki hata waandishi wa habari.


Kocha huyo raia wa Cameroon, amekuwa akiwaangalia wachezaji wake Watanzania na wale wa kigeni ambao wanawania kusajiliwa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV