July 3, 2016

CHANONGO AKISAINI MBELE YA KATIBU MKUU WA STAND UNITED, JONAS TIBOROHA.

Uongozi wa Stand United umeamua kukata mzizi wa fitna kuhusiana na usajili mpya wa kiungo wake Haruna Chanongo baada ya kumalizana naye leo.

Awali, kulikuwa na taarifa kwamba Chanongo alikuwa ametemwa lakini Katibu Mkuu wa Stand United, Dk Jonas Tiboroha akazungumza na SALEHJEMBE na kukanusha hilo, kwamba kuna kundi la watu wengine wanaojiita Stand ndiyo walitangaza.

Baada ya hapo, Stand imeamua kumsainisha Chanongo pamoja na wachezaji wengine ambao ni Saleh Mohammed na Edward Charles.CHALRES

SALEH MOHAMMED...

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV