July 15, 2016

OWUSU AKIHOJIWA JNIA

Baada ya kikosi cha timu ya Medeama kuwasili nchini kikitokea Ghana, kocha mkuu wa kikosi hicho, Prince Yaw Owusu, amefunguka kuwa anawajua vizuri wapinzani wake, Yanga, hivyo ana uhakika wa ushindi.

Medeama ilitua jana mchana kwa ajili ya mchezo wao wa kesho Jumamosi dhidi ya Yanga wa Kombe la Shirikisho Afrika unaotarajiwa kupigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.

Msafara wa Medeama una watu 32 ambao ni wachezaji 19, viongozi wa benchi la ufundi sita, waandishi wa habari wawili na viongozi wengine watano.

Akizungumza jana na muda mfupi baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Owusu alisema hii si mara yake ya kwanza kuja Tanzania kwa kuwa miezi michache iliyopita alikuja na kikosi cha Al Khartoum cha Sudan kwenye michuano ya Kombe la Kagame.

“Naijua Yanga vizuri tu kwani miezi michache iliyopita nilikuwa hapa na kikosi cha Al Khartoum kwenye Kagame nikiwa kocha msaidizi huku kocha mkuu akiwa ni Kwesi Appiah.

“Lakini kwa wachezaji wangu wote hii ni mara yao ya kwanza kuja hapa, lakini tumejiandaa kwa mapambano ili kuondoka na pointi zote tatu ambazo ndizo tunazihitaji kufikia malengo yetu ya hapo baadaye kucheza nusu fainali,” alisema Owusu.


Naye nahodha wa kikosi hicho, Mohammed Muntari Tagoe ambaye ni kipa alisema wamekuja kushindana na wale wanaowabeza basi wasubiri kuona kitakachotokea uwanjani.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic