July 13, 2016


Uongozi wa klabu ya Yanga umetangaza viingilio vya Sh 3,000 kwa sehemu zote na Sh 10,000 kwa VIP B na C wakati Yanga ikiivaa Medeama ya Ghana.

Kwa majukwaa ya orange itakuwa Sh 5,000. Na Sh 15,000 kwa VIP A.

Timu hizo zinakutana Jumamosi katika mechi ya Kombe la Shirikisho.

Awali, mashabiki wengi waliamini ingekuwa bure tena kama ilivyokuwa katika mechi kati ya TP Mazembe dhidi ya Yanga.

Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga, Baraka Deudetis amesema wameamua kuweka viingilio vya chini kabisa ili wajitokeze kwa wingi.

“Lengo ni kuomba mashabiki wajitokeze kwa wingi zaidi ili kupata ile dhana ya mchezaji wa 12. 


“Tunawaomba wajitokeze kwa wingi na kushangilia na ikiwezekana washangilie mwanzo hadi mwisho,” alisema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV