July 13, 2016


Mshambuliaji Amissi Tambwe ameanza mazoezi na kuamsha matumaini ya kuimarisha safu ya ushambulizi ya Yanga kabla ya Jumamosi.

Yanga ina kibarua cha kuivaa Medeama ya Ghana katika mechi ya Kombe la Shirikisho itakayopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Jumamosi.

Medeama itawasili nchini kesho saa 2 asubuhi na kufikia katika hoteli ya Protea, ikiwa tayari kuwavaa Yanga.

Tambwe ameanza mazoezi leo kwenye Uwanja wa Boko Veterani wakati Yanga ikifua. Alikuwa nje akijiuguza na ugonjwa wa malaria.

Inaonyesha bado Kocha Hans van der Pluijm ana nafasi ya kumtumia ingawa ni kwa asilimia 50 hadi sasa.

Lakini wachezaji majeruhi kama Deus Kaseke aliyepata ajali ya pikipiki, Haji Mwinyi na Geofrey Mwashiuya wanaonekana wataikosa mechi ya Medeama kwa kuwa ni majeruhi na hawakuwa wameanza mazoezi hadi leo.
0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV