July 9, 2016


Beki Hassan Kessy amerejea mazoezini Yanga kama ilivyo kwa mshambuliaji, Obey Chirwa raia wa Zambia.

Kessy aliamua kuacha mazoezi siku kadhaa ili kushughulikia suala lake na klabu ya Simba ambayo imemuwekea ngumu.
Wakati Chirwa alirejea kwao Zambia kukamilisha mambo kadhaa ambayo yalielezwa ni ya kifamilia.

Wawili hao, walikuwa mazoezini wakijifua na wenzao jana jioni, wakionyesha kuwa katika hali nzuri na tayari kwa kazi.
Chirwa na Kessy walionyesha wepesi na kufanya wawe kivutio kwa mashabiki waliojitokeza kuwashuhudia mazoezini.


Tayari Chirwa ameichezea Yanga mechi moja dhidi ya TP Mazembe wakati Kessy bado hajacheza kwa kuwa Simba bado inaendelea kuweka ngumu kwa madai alisaini mkataba na Yanga kabla ya ule aliokuwa nao kwisha.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV