July 8, 2016


NAHODHA WA SIMBA, MUSSA HASSAN MGOSI AKIWA NA WAKONGOMANI, BUKUNGU (KULIA) NA NDUSHA AMBAO MWENYEWE ANAONYESHA KUVUTIWA NA KAZI YAO.

Wakongomani Besala Janvier Bukungu na mwenzake Moussa Ndusha wameendelea kuonyesha uwezo mkubwa katika mazoezi ya Simba.

Wawili hao, wako nchini katika harakati za kujiunga na Simba ambayo imepania kuimarisha kikosi chake vilivyo.

Simba chini ya Kocha Mcameroon, Joseph Omog inafanya mazoezi kwenye uwanja ambao hawaruhusiwi mashabiki wala waandishi wa habari.

Lakini kwa mujibu wa wanaoshuhudia mazoezi hayo, wamesema beki ambaye ni Bukungu na kiungo Ndusha wameonyesha uwezo wa juu kabisa.0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV