July 16, 2016MPIRA UMEKWISHAAA
-Chirwa anaingia na kupiga krosi nzuri kabisa, lakini Ngoma anaonekana kutokuwa na nguvu ya kumalizia
-Ngoma anaingia vizuri, anakwenda anaanguka mwenyewe akionekana kuwa amechoka
-Yanga wanafanya kosa kosa lka mwaka, Abbas Mohammed aliyeingia kipindi cha pili anabaki yeye na kipa Dida lakini anashindwa kufunga, hii ni bahati kubwa kwa Yanga
-Yanga wanafanya shambulizi tena lakini Medeama wanaokoa

DAKIKA 5 ZA NYONGEZA
Dk 90, Medeama wanafanya shambulizi kali ndani ya eneo la hatari la Yanga wakigongeana vizuri lakini Bossou anaokoa na Dida anadaka vizuri
DK 87 hadi 89, Yanga wanafanya mashambulizi, lakini wanaonekana kuishiwa maarifa. Maana wanapiga krosi ambazo hazina manufaa lakini wanaendelea kupiga krosi tena na tena
 Dk 86, Yanga wanajichanganya, Twite anampa adui mpura, anaingia vizuri Kwame na kupiga shuti, hata hivyo anashindwa kulenga lango
Dk 85, Medeama bado wanaonekana kupoteza muda wakitaka sare huku Yanga wakionekana kuwa na presha wakitaka kupata bao la pili

Dk 84, Mahadhi anajaribu kuwatoka mabeki wa MEdeama lakini Adade anawahi na kuokoa
Dk 82, Niyonzima anapokea pasi ya Mahadhi, anageuka haraka na kupiga shuti kali, lakini mabeki Medeama wanakoa tena
Dk 80, Yanga wanagongeana vizuri, Mahadhi anauwahi mpira wa Niyonzima na kupiga shuti kali, kipa Medeama anaonyesha ujuzi na kuokoa tena
SUB Dk 77, Yanga wanamtoa Joshua na nafasi yake inachukuliwa na Haruna Niyonzima. Hii maana yake Twite anashuka kwenda kucheza namba tatu, Kamusoko anashuka sita na Niyonzima anakwenda nane

SUB Dk 76, Juma Mahadhi anaingia kuchukua nafasi ya Amissi Tambwe
Dk 73, krosi nyingine safi kabisa ya Juma Abdul, mabeki Medeama wanajichanganya lakini hakuna mtu pale, wanaokoa tena
Dk 73, unaweza ukadhani utani, Yanga wanapoteza nafasi nyingine tena ya wazi kabisa. Ngoma ndani ya eneo la 18, kipa ndiyo pekee mbele yake, anashindwa kufunga kwa kichwa

Dk 70, Kamusoko anaanchia shuti kali kabisa, kipa Medeama anaonyesha ujuzi hapa na kuutoa, kona. Yanga wanapiga lakini haina madhara
Dk 69, Yanga wanamuacha Kwake aingie peke yake, hayuko mbali sana na lango anapiga shuti lakini linapita juu ya lango la Yanga
Dk 65, Msuva anakwenda kuzozana na kipa wa Medeama akitaka mfuko wa kipa aliouweka ndani ya lango uondolewe, mwamuzi anamsikia na kumwamuru kipa huyo aende kuutoa na kuuweka nje ya lango

Dk 64, mpira umesimama takribani dakika moja,beki Aidoo wa Medeama akiwa chini, akidai alichezewa rafu
Dk 62 Yondani anapanda na kupiga pasi nzuri, Yanga wanafanya shambulizi na krosi nzuri ya Juma Abdul lkakini Medeama wanaokoa tena
Dk 59, Juba Abdul anaingia na kupiga krosi safi kabisa, Ngoma anaunganisha kwa tik tak lakini kipa anaokoa vizuri kabisa
Dk 54 hadi 57, Yanga wanaonekana kutulia vizuri na kucheza pasi mpira wakiwa nao, lakini bado hawajafanya shambulizi kali hata mara moja
Dk 52, Tambwe anaingia vizuri tena, anampa mpura MSuva lakini Medeama wanaokoa vizuri

Dk 50, Medeama wanaingiza mpira mzuri ndani ya lango la Yanga lakini Yondani anawahi na kuokoa
Dk 48, Tambwe anapoteza nafasi nzuri kabisa, anabaki yeye na kipa na kushindwa kufunga, nini hiiii
Dk 46 Mpira unaanza taratibu lakini Ngoma anamwangusha mshambulizi wa Medeama
MAPUMZIKO
DAKIKA 2 ZA NYONGEZA
Dk 44, Yanga wanaanza kushambulia tena, lakini bado hakuna mashambulizi makali kwakuwa aina yao ya uchezaji ni kupiga mipira mirefu na Ngoma amethibitiwa
Dk 42, Twite anamwangusha mshambuliaji wa Medeama ambaye alimtoka Bossou kwa kasi kubwa, lakini mwamuzi anamsamehe

Dk 39, Bossou anaanguka wakati akiwania mpira na Kwame, lakini pamoja na janja yake analambwa kadi ya NJANO.
Dk 37, Medeama wanapata kona, wanachonga na wao wanauwahi na kupiga na unatoka kidogo nje ya lango la Yanga. Hili ni kosa kama lililozaa bao la kwanza
Dk 35, Chirwa anamgeusa Aidoo wa Medeama nakubaki yeye na kipa lakini anampa mikononi

Dk 33, Tambwe anapiga kichwa tena lakini unakuwa mpira lahisi kwa kipa wa Medeama
Dk 32, Oscar Joshua anaingiza krosi safi kabisa lakini moira unampita Tambwe
Dk 31, Dida anajitokeza na kudaka vizuri mbele ya Kwame. Kinachoonekana Yanga wana tatizo la kiungo na wanapoteza mipira mipingi sana

Dk 29, Juma Abdul ananusurika kulambwa kadi ya njano baada ya kumchezea kindava Kwame wa Medeama
Dk 28 Yanga wanaonekana kuamka krosi ya Juma Abdul lakini Medeama wako makini zaidi

Dk 22 hadi 25, Medeama wanaonekana kushambulia zaidi kuliko Yanga na wakicheza kwa kujiamini
Dk 20, Medeama wanafanya shambulizi jingine na Yondani anajitokeza na kuokoa
GOOOOOO Dk 17, Benard Danso anaifungia Medeama bao la kusawazisha baada ya kuunganisha mpira wa kona akiwa mbele ya Bossou

Dk 12 hadi 15, Medeama wanaonekana kuchezea zaidi upande wa Yanga na wanalazimika kuwa makini
Dk 11, Yanga wanalazimika kuokoa tena baada ya Kwaeme kumpa pasi nzuri Adade lakini hata hivyo hawakuwa makini

DK 8, MEdeama wanaingia vizuri kwenye lango la Yanga, kinachoonekana hapa ni kama Yanga wanafanya mzaha. Yanga waliokoa lakini Yondani akaanguka na Medeama wanapata nafasi aya kupiga shuti
Dk 4, Kamusoko anaingia vizuri tena na kutoa paso lakini Tambwe anashindwa kumalizia
GOOOOOOOO DK 1 Ngoma anaipatia Yanga bao safi baada ya Msuva kuingia na kupiga pasi safi kabisa

KIKOSI 01. Deo Dida
02. Juma Abdul
03. Oscar Joshua
04. Kelvin Yondani
05. Vicent Bossou
06. Mbuyu Twite
07. Simon Msuva
08. Thabani Kamusoko
09. Donald Gnome
10. Amissi Tambwe
11. Obey Chirwa

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV