July 16, 2016


Huku kambi ya Simba ikizidi kuchanganya huko mkoani Morogoro, kocha msaidizi wa timu hiyo, Jackson Mayanja, amesema kikosi chao kitakuwa moto msimu ujao kwani kina wachezaji sahihi kuliko msimu uliopita. 

Kauli hiyo ya Mayanja raia wa Uganda inakuja wakati kocha mkuu wa timu hiyo, Joseph Omog akisisitiza zaidi wachezaji kuwa na stamina itakayowawezesha kupambana dakika zote uwanjani. 

Mayanja amesema, mwanga umeanza kuonekana na anawapongeza viongozi kwa kusajili wachezaji ambao aliwapendekeza.

“Tutakuwa moto sana msimu ujao kwa sababu kikosi chetu kimejaa wachezaji walio na viwango ambao niliwaomba viongozi wawasajili.

“Kikubwa ambacho tunataka ni tupewe muda tu wa kuingiza ufundi wetu na Simba mbona itarejea kwenye mstari wake,” alisema Mayanja.


Wakati huohuo, katika mazoezi ya Simba kambini Morogoro, Kocha Omog ameonekana kuvalia njuga mazoezi ya fiziki ili kuwaongezea stamina wachezaji wake.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV