July 23, 2016



Siku za nyuma kidogo hali ya uoga iliitwa kuchachawa, sasa Medeama SC ya Ghana imechachawa na kuiomba Bodi ya Ligi Kuu ya Ghana kuahirisha mechi yao moja ya Ligi Kuu Bara ili ijiandae kuivaa Yanga.

Baada ya sare ya bao 1-1, wikiendi iliyopita jijini Dar es Salaam, Medeama itarudiana na Yanga, Jumanne ijayo jijini Accra, Ghana katika mchezo huo wa Kundi A la Kombe la Shirikisho Afrika.

Kutokana na umuhimu wa mchezo huo, Medeama imeomba na kuruhusiwa kutocheza mechi yake ya ligi kuu iliyopaswa kuchezwa leo Jumamosi dhidi ya Wa All Stars.

Kwa mujibu wa habari kutoka Ghana, Medeama ndiyo waliopeleka maombi ya mchezo huo usogezwe mbele ili waweze kujiandaa vizuri chini ya Kocha Pride Owusu.

Mara baada ya Medeama kukabidhi barua ya maombi hayo, bodi ya Ligi Kuu ya Ghana ilikubali na kuipa nafasi zaidi timu hiyo kujiandaa na mechi dhidi ya Yanga, pia kuwapa wachezaji muda wa kutosha wa mapumziko.

Katika ligi kuu, Medeama ipo nafasi ya tatu ikiwa na pointi 33 katika mechi 19 ilizocheza na inaonekana inaweza kufanya vizuri hivyo kuwa na matumaini ya kushiriki tena Michuano ya Shirikisho la Soka Afrika (Caf) msimu ujao.


Katika Kundi A, Medeama inashika nafasi ya tatu ikiwa na pointi mbili huku Yanga ikiwa mkiani na pointi moja wakati TP Mazembe ikiwa kileleni na pointi saba na MO Bejaia ni ya pili na pointi tano. Timu zote zimecheza mechi tatu.

1 COMMENTS:

  1. Huku akina Wambura waligoma kusogeza mechi ya yanga na Mtibwa,hata pale Ndanda walipoombwa kucheza Dar bado kukawa na figisu za ajabuajabu!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic