July 7, 2016Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano cha Yanga, Jerry Muro amefungiwa mwaka mmoja kujihusisha na masuala ya soka.

Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), imetangaza kumfungia Muro kupitia ile kesi yake kwamba amekuwa akiipinga na kuishambulia TFF kwenye vyombo vya habari.

Kikao cha Kamati ya Maadili ya TFF, kilikaa leo bila ya Muro kuwepo kwa kuwa wakati mwaliko unatoka alikuwa nje ya Dar es Salaam.

Katika makosa matatu aliyoshitakiwa, moja amekumbana na adhabu hiyo, moja amepigwa faini ya Sh milioni 3 na moja ameonekana hana hatia.

Awali Muro alisema alikuwa mapumzikoni Machame mkoani Kilimanjaro ambako ni kwao.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV