July 7, 2016


Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm ameeleza sababu ya mazoezi ya Yanga kuwa ya nguvu kazi utafikiri mechi.

Pluijm raia wa Uholanzi, amesema lazima mazoezi yawe magumu ili kuhakikisha yanaenda na uhalisia.

“Tunahitaji kucheza kwa kasi, kwa nguvu. Tunashambulia na kulinda pamoja. Haya yote lazima yafanyike mazoezini. Uhalisia ndiyo unatengeneza ubora sahihi,” alisema Pluijm.

Katika mazoezi ya Yanga, wachezaji wamekuwa wakicheza ngangari kweli utafikiri ni mechi hasa.


Baadhi wamekuwa wakipata hofu huenda wanaweza kupata majeraha lakini mazoezi hayo yamekuwa yakisifiwa na mashabiki kwamba ni mazoezi hasa na hakuna utani.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV