July 9, 2016

Hafla ya kukabidhi tuzo mbalimbali za washindi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwa msimu wa 2015/2016 itafanyika Julai 17 mwaka huu.

Jumla ya tuzo 13 za Ligi hiyo inayodhaminiwa na kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania zitatolewa katika hafla itakayofanyika Julai 17 jijini Dar es Salaam, na kuratibiwa na Kamati ya Tuzo ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).


Kamati hiyo inaundwa na waandishi wa habari za michezo, makocha, viongozi  (administrators) na wawakilishi kutoka kwa wadhamini (Vodacom na Azam Tv).

Huku beki wa Azam FC, Serge Wawa ambaye hakuwa na msimu mzuri akikosa nafasi hiyo, wachezaji waaliongia kwenye orodha ya tuzo ya mchezaji bora wa kigeni ni Donald Ngoma (Yanga), Thabani Kamusoko (Yanga) na Vincent Agban (Simba). 

Tuzo nyingine zitakazotolewa katika hafla hiyo ni mabingwa, makamu bingwa, mshindi wa tatu, mshindi wa nne, timu yenye nidhamu, mfungaji bora, mchezaji bora wa Ligi, kipa bora, kocha bora, mchezaji bora chipukizi, mchezaji bora wa kigeni, goli bora la msimu na mwamuzi bora.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV