July 9, 2016


Hafla ya kukabidhi tuzo mbalimbali za washindi wa Ligi Kuu Bara msimu wa 2015-16, wachezaji kutoka Azam FC, Simba na Mtibwa Sugar ndiyo watakowania tuzo ya Mwanasoka Chipukizi wa ligi hiyo.

Waliopendekezwa kuwania tuzo ya mchezaji bora chipukizi ni Farid Mussa (Azam), Mohamed Hussein Zimbwe (Simba), Mzamiru Yasin (Mtibwa Sugar) na Shiza Kichuya (Mtibwa Sugar).

Hafla ya utoaji tuzo itafanyika  itafanyika Julai 17 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Jumla ya tuzo 13 za Ligi hiyo inayodhaminiwa na kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania zitatolewa katika hafla hiyo itakayofanyika jijini Dar es Salaam, na kuratibiwa na Kamati ya Tuzo ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

Kamati hiyo inaundwa na waandishi wa habari za michezo, makocha, viongozi  (administrators) na wawakilishi kutoka kwa wadhamini (Vodacom na Azam Tv).

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV